Monday 8 February 2016

Kwa Mara ya Kwanza Kocha Jose Mourinho Aongelea Kuhusu Kurudi Uwanjani Kufundisha Baada ya Kufukuzwa Chelsea

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kwa kocha wa zamani
wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, February 7 karudi
kwenye headlines na kauli mpya baada ya kutokuwa tayari
kuzungumzia soka, Jose Mourinho ameamua kuzungumzia
soka ikiwa ni wiki sita zimepita toka afukuzwe kazi na
Chelsea.
Jose Mourinho ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na
Man United ili arithi nafasi ya Louis van Gaal alikuwa hayupo
tayari kuzungumzia soka, ila kwa sasa amekubali
kulizungumzia hilo na kukiri kuwa yupo karibu kurudi kazini
hivi karibuni, licha ya kuwa wengine huwa wanamtafsiri kama
jeuri, lakini yeye anasema ni mtu wa kawaida na anajifunza
popote.
“Siku zote nimekuwa nikijifunza hata katika sehemu
ambayo najihisi ni mtaalam, siku zote mimi sio
mkamilifu na nimekuwa nikijifunza kila siku, wakati
mwingine katika kazi na hata maisha binafsi, narudi
karibuni katika soka sehemu ambayo nahisi ni maisha
yangu ya asili” Jose Mourinho


0 comments:

Post a Comment