Monday 17 September 2018

🌹ADABU YA MUME KWA MKEWE.🌹


Usitangaze udhaifu wa mkeo kwa familia na marafiki, kila mmoja anamtunzia mwenziwe hadhi yake.

Usiwe na mtizamo mbaya wala kuzungumza naye kwa hisia kali huwezi kujua atatafsiri vipi.!!

Usimlinganishe mkeo na wanawake wengine, huwezi kujua hao wanawake wengine wanapitia hali gani kimaisha, kila mwanamke anasifa zake.

Usisahau kwamba ni mkeo umemuoa, yeye si kijakazi, muhudumie kama malikia na atauonyesha ulimwengu kwamba Mumewe ni mfalme na utamtawala maishani.

Mpe kipaumbele na ni wajibu wako binafsi kumfanyia jambo na sio watuwengine.

Usimlaumu mbele za watu hata kama kakosea, mlinde, muhimize, mrekebishe faraghani, ukifanya hivyo kamwe hatokusahau.

Usimnyime huduma za kitandani kwa kujifanya mgonjwa/kuchoka ama kutokuwa na hamu, kumbuka wanaume wengine wanatafuta nafasi hiyo.

Usimlinganishe mkeo na mtalaka wako ama mkeo aliyefariki maana wewe ni mume wa pekee kwake.

Usimkemee wala kumkosoa mbele ya watoto, ni malezi mabaya kwa watoto maana wewe ni mwalimu wao, wanakutazama wewe japo unadhani ni watoto tu!!.

Mtazame mkeo kama kavaa vizuri kabla hajatoka maana akipendeza yeye na wewe unaheshimika na ukipendeza wewe yeye anaheshimika.

Usikubali marafiki kuwa karibu na mkeo, weka mipaka maana hujui nia zao.

Usitoke kuoga na haraka haraka ukavaa nguo ukatoka pasi yeye kukukagua, mkeo kazungukwa na wanaume wanadhifu wanaojali mavazi na utanashati.

Wazazi, ukoo na marafiki sio waamuzi kwa mambo ya mkeo, usipoteze muda kutafuta uamuzi wa mwisho kutoka kwao, ithibiti ndoa yako.

Mapenzi yako yasiwe kwa sababu ya mazingira au kihali hata kama ulimuoa kwa misingi hiyo kwa sasa ni mkeo mpende bila masharti, hali uweza kubadilika na ikiwa ndio msingi basi ndoa itavunjika.

Mkeo anahitaji umakinike kwake na umsikilize kama mtoto, usiwe mkali msikilize kwa makini na atakupenda.

Usijilinganishe na mkeo, yeye ni mke kwa hivyo msaidie tu maanandoa ni kusaidia.

Usimuhukumu mkeo, ni msaidizi wako na kiumbe dhaifu mchukulie kwa mtazamo huo na utapata utulivu wa akili.

Mume mzembe hajali, haogi, jiweke nadhifu ukiwa na yeye nukia vizuri, harufu mbaya inamkirihisha ila hawezi kukwambia.

Usiwe na urafiki na waume walio na mtazamo mbaya kuhusu ndoa. Watakuharibu mawazo.

Mkeo ana thamani kubwa sana ndio maaana ukatoa vitu vya thamani kumuoa, penzi lenu lifanye jipya, uzembe haufai.

Kuzaa ni majaaliwa, mpende mkeo awe na watoto au asiwe nao, usiwabague watoto kwa jinsia wafunze dini na watakuwa wacha Mungu hadi maishani mwao.

Hauwi mzee kwa mkeo katika kumburudisha, usiwe na ugomvi naye mutakuwa katika kheri, usiwache kuwajali watoto wako na mkeo kwa sababu ya wanawake wengine au sababu yoyote ile, wao ni wewe na wewe ni wao.

Mume anayedumu na ibada ana usalama, omba kila siku, muombee mkeo na watoto.

Ukijiunga na group letu la UISLAMU CHAGUO LANGU na kulike page yetu ya Habari za kiislamu na kututembelea Furaha ya Ndoa utaelimika na ndoa yako.

💕TUKIYAFANYA HAYA TUTAKUWA NA NDOA BORA MNO!!💕

1 comments: