Wednesday 8 October 2014

MSAFARA WA MGONJWA WA EBOLA NI ZAIDI YA RAISI

Kuna Nesi mmoja amegudulika kuwa na
ugonjwa wa Ebola baada ya kuwahudumia
Wamishionari wawili waliokua na ugonjwa huo
baada ya kutoka nao Sierra Leone walikokua
wamekwenda kujitolea kufanya kazi.
Ugonjwa wa Ebola imekua ishu kubwa kwenye
hizi nchi maarufu duniani ambazo zimejikuta
zikiingia kwenye headlines kwa Wagonjwa
kuanza kupatikana ambapo Marekani kuna
mmoja aliingia na Ebola kutokea Afrika na
mwingine ni huyu Nesi wa Hispania.
Labda unaweza kushangaa ni jinsi gani huyu
Nesi amekua akilindwa baada ya kujulikana
amepata huo ugonjwa, hiyo picha ya juu hapo
sio msafara wa Kiongozi bali ni Polisi walikua
wanamsindikiza Nesi huyo kumpeleka Hospitali
ya Carlos III.
Baada ya kuugua Ebola Nesi huyu ambae bado
jina lake wala sura yake havijaonyeshwa
alisababisha Mume wake pamoja na watu
wengine 50 kuwa chini ya uangalizi ili kujua
kama na wao wameambukizwa lakini mpaka
Jumanne jioni (October 7) hakuna yeyote kati
yao aliekutwa na Ebola.

0 comments:

Post a Comment