Monday, 6 October 2014

BLATTER KUACHIA NGAZI FIFA

Mjumbe wa zamani wa shirikisho la soka duniani
amesema kuwa heshima ya Fifa haitaweza
kurudi mpaka pale Rais Wa shirikisho hilo Sepp
Blatter atakapoachia ngazi.
Michael Hershman ameiambia BBC kuwa Sepp
blatter hanabudi kuondoka na kupisha mtu
mwingine kukiongoza chombo hicho.
Amedai kuwa hivi sasa yanatakiwa mabadiliko ya
uongozi baada ya Fifa kuwa katika mlolongo wa
shutuma za rushwa kwa miaka mingi,hivyo basi
ni vyema uongozi ukabadilika.
Blatter amekuwa Rais wa shirikisho hilo tangu
mwaka 1998 na mwezi uliopita alitangaza nia ya
kuwania tena nafasi hiyo ingawa aliahidi kuwa
awamu ya nne ambayo ni sasa, ni ya mwisho.
Hershman amesema anasikitishwa mno na hatua
ya wadau wa nje hasa wadhamini kutoingilia kati
na kuchukua hatua stahiki, badala yake
wamekuwa wakitoa taarifa kwa vyombo vya
habari wakisema wanatarajia kuona FIFA
ikitekeleza majukumu yake kwa kufuata maadili.

0 comments:

Post a Comment