Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

Friday, 26 February 2016

Majina Ya Mawaziri MAJIPU Yakabidhiwa Kwa Waziri Mkuu......Ni Wale Waliogoma Kutangaza Mali Zao

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imemkabidhi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa majina ya baadhi ya mawaziri na naibu mawaziri ambao hawajajaza fomu za mali wanazozimiliki kama sheria inavyowataka.

Akizungumza jana kwenye semina ya mawaziri na naibu mawaziri, Kamishina wa Sekretarieti hiyo, Jaji mstaafu Salome Kaganda alisema viongozi hao wanajua umuhimu wake lakini wanapuuza.

“Sheria hii ya Maadili ya Viongozi wa Umma inajulikana, lakini jambo la kushangaza wapo baadhi ya mawaziri na manaibu ambao hawajajaza, kwa ruhusa yako nitakukabidhi majina yao, sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria, hivyo anayekiuka anapaswa kuadhibiwa,” alisema Jaji Kaganda bila kutaja majina hayo.

Kifungu cha 9 cha sheria hiyo kinataka katika kipindi cha siku 30 baada ya kupewa wadhifa, kila mwisho wa mwaka na mwisho wa kutumikia wadhifa wake kiongozi husika anatakiwa kupeleka tamko la maandishi la mali zake.

Sheria hiyo inafafanua kuwa mali hizo ni pamoja na rasilimali zake au mume au watoto wenye umri usiozidi miaka 18 ambao hawajaoa au kuolewa.

Alisema fomu hizo lazima zijazwe na viongozi na wananchi wanaruhusiwa kwenda kuzihakiki wakitoa sababu za msingi, lakini sheria hiyo hairuhusu waende kutangaza na wakifanya hivyo hatua zinachukuliwa dhidi yao.

“Hapo ndipo wananchi wengi huwa hawatuelewi kwa kuwa wanapenda kujua mali ambazo viongozi wao wanamiliki,” alisema.

Alisema Sekretarieti kwa kutambua umuhimu wa viongozi hao kuzingatia sheria na maadili, ndiyo sababu imeandaa semina hiyo baada ya kupata ufadhili kutoka Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID), wakiamini kuwa yatasaidia kuwakumbusha.

Ester Bulaya Atamba 'Nitaendelea Kumgaragaza Wasira Ubunge wangu si Wakuchakachua'


Mbunge wa Bunda Mjini, mkoani Mara, Esther Bulaya (Chadema), ametamba kuwa ataendelea kumshinda mpinzani wake kisiasa, Stephen Wasira (CCM), kwa madai kwamba alipata ubunge huo kihalali.

Bulaya alisema hayo jana ikiwa ni siku moja tangu kutupwa kwa rufaa ya wanachama wa CCM waliokuwa wakipinga ushindi wa mbunge huyo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 dhidi ya Wassira na wagombea wa vyama vingine.

Mbunge huyo aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake kuwa, alimshinda Wasira kwa wananchi, akamshinda kisheria, lakini hakuridhika akakata rufaa na ameendelea kumshinda.

"Kama ana mpango wa kukata rufaa nyingine aende akate tu, lakini akumbuke kuwa nitaendelea kumshinda tu kwa sababu ubunge wangu sio wa kuchakachua bali nimeupata kutokana na kura za wananchi wa Bunda Mjini," alisema Bulaya na kuongeza:

"Siku zote nimekuwa nikisema kuwa waliofungua kesi sio wanachama wa CCM bali ni Wasira mwenyewe, ndio maana akawa mkali kupigwa picha na waandishi ili Watanzania waendelee kudhani kwamba hayumo katika kesi hiyo," alisema.

Alisema wakati umefika sasa mwana siasa huyo mkongwe kupumzika na kula mafao yake, kwa kile alichosema ametumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni zamu ya wengine kumpokea kijiti ili kuanzia pale alipoachia.

"Pamoja na hayo ninamkumbusha kuwa siku zote mahakama husimamia haki ndio maana ameshindwa mara mbili katika kesi hii, hivyo hana budi kupumzika," alisema.

Januari 25 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wapigakura Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagira kupinga ubunge wa Bulaya.

Bulaya alihama CCM na kujiunga na Chadema katikati ya mwaka jana na kuteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini na kufanikiwa kumbwaga mkongwe huyo kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana

Monday, 8 February 2016

Mnyonge Mnyongeni Rais Magufuli Ndio Rais Tuliyokuwa Tunamtaka Tanzania...Ukweli Utabaki pale pale

Mungu ni mwema hatuna budi kumshukuru kwa anayotufanyia
katika nchi yetu.
Baada ya kusema hayo niseme bila kumung’unya maneno
kwamba Rais Dk. John Pombe Magufuli ndiye rais tuliyekuwa
tunamtaka kutokana na anachokifanya sasa.
Nichukue nafasi hii kumpongeza kwa hatua anazochukua ili
kuwafanya wananchi wanufaike na rasilimali za nchi hii, hivyo
namtakia kila la heri katika kazi yake ya kututumikia. Naomba
kukiri kwa uwazi kwamba Watanzania tulifanya chaguo sahihi,
hatukukosea.
Tanzania ina vyama 23 vya siasa vilivyosajiliwa na
vinavyofanya kazi sasa, tutake tusitake Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kilimuona Dk. Magufuli kuwa ni tunu ya taifa na leo
anadhihirisha hilo kwa kupigania wananchi wake na kuwa adui
kwa mafisadi.
Kila Mtanzania sasa anaamini kwamba Dk.Magufuli anaweza
kurejesha bila wasiwasi usimamizi thabiti wa serikali na
nidhamu ya utendaji ndani ya serikali. Naamini kuwa serikali
ya Magufuli itakuwa ya kiusimamizi na yeye mwenyewe
anaweza kulifanya jambo hilo bila kusita. Tumeona.
Katika nyadhifa nyingi alizopitia hadi sasa ameijenga taswira
hii kila alikopita na bado inambeba katika awamu hii ya
tano.Hakuna siri, kama kuna jambo ambalo lilikuwa haliendi
sawa nchini ni la utendaji ndani ya serikali. Tunafahamu kuwa
wafanyakazi ndani ya serikali ukiachilia mbali matatizo
waliyonayo kwa maana ya vipato, hata mambo madogo
ambayo wangeweza kuyasimamia ndani ya dakika au saa
chache yalichukua wiki hata miezi kadhaa.
Utaratibu wa utoaji huduma ulikwama sana lakini kwa spidi ya
Rais Magufuli atafanikiwa kutatua changamoto hiyo kubwa na
ya siku nyingi. Ikiwa utendaji wa serikali unaimarika na
huduma zinatolewa kwa wakati, tutaweza kujenga taifa
linalokwenda mbele kimaendeleo.
Taswira bora ya pili ya serikali ya Dk. Magufuli ni misimamo
katika masuala ya msingi na kutoyumba. Magufuli muda wote
ambao amekuwa kiongozi anaonesha njia, ndiyo maana
alipoanza tu kazi, alianza na tabia ya ziara za kushtukiza. Hii
alikuwa akifanya hata alipokuwa waziri wa ujenzi.
Moja ya mambo ambayo serikali iliyopita ilikosa ni pamoja na
kukosa misimamo na kuwa na Double standard. Mfano
mdogo tu ni kwenye mchakato wa Katiba Mpya ambapo rais
anayeondoka alisimamia uanzishwaji bora wa mchakato huo,
akaunga mkono katika hatua zote na rasimu zote, lakini akaja
kuwageuka wajumbe wa tume hiyo na rasimu yao ya pili
alipolihutubia Bunge Maalumu la Katiba.
Naamini Magufuli si mtu wa kugeuka na kuna masuala mengi
anaweza kuyasimamia kwa dhati na kila mmoja wetu
akakubali kuwa, huyu ni kiongozi anayesimamia haki na ana
uchungu na wananchi wake.
Amekuwa akitetea wanyonge hadharani mara nyingi na
anaonekana wazi kwamba anaumizwa na watu wanaoibia
serikali bila kujali kuwa kuna watu wanakosa mlo mmoja kwa
siku.
Wote tumuunge mkono, ni rais anayestahili sifa hizo,
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa kufanya
hivyo naamini tutashinda.
Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.


Friday, 29 January 2016

NAPE KUPELEKWA MAHAKAMANI?


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kufuatia kauli ya Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyotolewa jana bungeni, atapeleka hoja kwa wananchi ili kuona kitendo hicho kama kinakubalika ama la.
Alisema hayo leo katika Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanahabari, akisema kutorusha matanagzo hayo ‘live’ ni kumnyima mtanzania haki yake ya msingi kwa kuwa matangazo hayo yanalipiwa na kodi za wananchi wenyewe.
Alisisitiza kuwa haiwezekani kurushwa baadhi ya vipengele, tena nyakati za usiku, muda ambao televisheni nyingi huonyesha vipindi vya burudani na wananchi wengi pia huwa wamechoka kutokana na kazi.
Aliitaka serikali kutaja kiasi cha fedha zinazotakiwa kurusha matangazo hayo ‘Live’ ili atakapopeleka hoja yake kwa wananchi, wakikubali kuchangia, wajue ni kiasi gani kitatakiwa ili hata kama TBC itakataa, wapeleke kwenye televisheni nyingine.

Monday, 25 January 2016

Uamuzi wa Kufuta Uchaguzi Zanzibar Wazidi Kukosolewa..Mwanasiasa Mwingine Mkongwe Atoa ya Moyoni

Uamuzi wa Kufuta Uchaguzi Zanzibar Wazidi Kukosolewa..Mwanasiasa Mwingine Mkongwe Atoa ya Moyoni

Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo.
Amesema jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo, amesema kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema.
Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana.  Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi  wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza  wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao. “Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutwa kumewashangaza wengi na bado suala hili halieleweki. “Pia hili jambo sidhani kama ni la mtu mmoja…sidhani kama ni la Jecha peke yake. Huu si mustakabali mzuri kabisa, Zanzibar ni nchi ndogo, lakini ina historia kubwa kisiasa hivyo juhudi za pamoja zifanyike kutatua mgogoro huu kwa matakwa ya Watanzania kwa ujumla.

Monday, 18 January 2016

Wabunge Wote wa CCM Wakutana Dodoma Kupanga Mikakati..Nimekuwekea Picha Kadhaa Hapa


Wabunge wa CCM wakimsikiliza Mbunge wa Kibakwi Mhe. Boniface Simbachawene wakati akifafanua mambo mbali mbali kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William Lukuvi akichangia hoja kwenye semina ya wabunge wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) ambaye ndie mwenyekiti wa kikao maalum chenye kutoa semina elekezi kwa wabunge wa CCM, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto).
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba akifuatilia kwa makini hoja mbali mbali zilizotolewa na wabunge wa CCM kwenye semina maalum elekezi kwa ajili ya wabunge wa CCM mjini Dodoma

Magazeti ya Leo » Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Januari 19, Ikiwemo ya Lowassa Kutamba Kuwa Mtaiona Dar ya Ukawa


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Januari 19, Ikiwemo ya Lowassa Kutamba Kuwa Mtaiona Dar ya Ukawa

Thursday, 14 January 2016

Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Wakili wa Serikali


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika jana Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Januari 11, 2015 katika mahakama hiyo.
Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;
 Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria
Katika uamuzi wa MAHAKAMA, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;
 Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo
Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea Januari 28, 2015.

Edward Lowassa Atangaza kugombea tena Urais Mwaka 2020, asisitiza yupo fiti

Akiongea na wafanyabiashara wa kariakoo waliomtembelea ofisini kwake mikocheni, Lowassa amesema safari ndio kwanza imeanza na yupo fiti kwa mapambano.
Amewataka wanamabadiliko kutokukata tamaa 
Amesisitiza kama alivyoshinda uchaguzi huu ndivyo atakavyoshinda mwaka 2020.

Tundu Lissu: Viatu vya Dk. Slaa Vikubwa Kumpata wa Kuvivaa Ipo Shughuli

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA amesema kuwa viatu vya Dkt. Slaa ni vikubwa, hivyo kupata mtu wa kuvivaa na vikamuenea ni ngumu
Amesema Mwenyekiti wa Chama ndiye mwenye mamlaka ya kumchagua mtu anayeona ana uwezo wa kutosha wa kukiongoza chama kwa nidhamu

Wednesday, 13 January 2016

Nape Atoa Mpya..Aitaka Chadema Kumfukuza Edward Lowassa


CCM imemjibu mwanasheria Mkuu wa Chadema ikisema ili chama hicho kikuu cha upinzani kionekane kinapambana na ufisadi kwa vitendo, kinatakiwa kumuunga mkono Rais John Magufuli na kumvua uanachama Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye alisema Chadema iliachana na ajenda ya kupambana na ufisadi baada ya kumpokea Lowassa  Julai mwaka jana baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa CCM kusaka mgombea wake wa urais.
“Sisi hatukumpitisha (Lowassa) awe mgombea wetu wa urais kwa sababu hiyo (ya ufisadi) na ndiyo maana yeye mwenyewe aliamua kuondoka na kwenda Chadema,” alisema Nape.
“Hata katika kampeni za uchaguzi mkuu, Chadema hawakuzungumzia ajenda ya ufisadi, ni kama Lowassa aliifunika tu.”
Alikuwa akimjibu Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye  juzi alisema ufisadi ni ajenda ya kudumu ya chama hicho kwa kuwa Rais Magufuli hataweza kuufumua wote katika kipindi cha miaka mitano.
Huku akichelea kueleza kiundani sababu za CCM kutomfukuza Lowassa kwa tuhuma za ufisadi mpaka alipoamua kujiondoa na kujiunga na Chadema, alisema kauli ya Lissu inalenga kuwahadaa Watanzania.
“Kauli ya Lissu ni ya kushangaza sana. Sisi tunajua jinsi ambavyo Chadema na washirika wake walivyojitenga na ajenda ya ufisadi. Kama kweli wanaupinga, basi wamuunge mkono Rais Magufuli ambaye kwa sasa anapambana na ufisadi kwa kasi,” alisema mbunge huyo wa Mchinga.
“Wakati mwingine kila jambo hufanyika kwa wakati wake. Suala la kupinga ufisadi CCM lilianza siku nyingi tangu enzi za kujivua gamba. Tumeendelea nalo mpaka watu wakajiondoa wenyewe,” alisema Nape.
Alisema hoja ya kupinga ufisadi ndani ya CCM ilikibeba chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kikapata ushindi mnono, huku Chadema iliyokuwa ikilia na ufisadi ikishindwa.
 “CCM tulieleza sababu za kutompitisha Lowassa kugombea urais na hilo lilikuwa wazi,” alisema.
Katika ufafanuzi wake wa juzi, Lissu alisema ili apambane na ufisadi, Rais Magufuli anapaswa kuacha tabia za CCM na kumtaka mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) amtangaze mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu ambao Chadema wanaamini Maalim Seif Sharif Hamad alishinda.
Pia Lissu alimtaka Rais ataje majina ya waliokwepa kodi ili kama watajitokeza kuwania uongozi, wadhibitiwe kwa kuwa Katiba imezungumza kwa maneno makali dhidi ya vitendo hivyo viovu.
Aidha, aliponda uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo anayetajwa kuhusiska katika sakata la uchotwaji wa Sh3060 bilioni kutoka akaunti ya Tetega Escrow.
Miaka 39 ya CCM
Akizungumzia maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, Nnauye alisema uzinduzi utafanyika Januari 31, visiwani Zanzibar na mgeni rasmi atakuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.
Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa Februari 6, mjini Singida na yataongozwa na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye aliiongoza Serikali ya Awamu ya Nne.
“Viongozi wa kitaifa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria maadhimisho haya watapangiwa shughuli za ujenzi wa chama na taifa katika wilaya zote za mkoa wa Singida, siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho,” alisema.
Alisema mikoa yote nchini inapaswa kuandaa shughuli hiyo wiki moja kabla ya maadhimisho, na kwamba lengo ni kufanya shughuli za ujenzi wa chama hicho katika maeneo yao.
“Tutakachokifanya wiki hiyo ni kupokea wanachama wapya, kufanya mikutano ya kuwashukuru wananchi kwa kuiamini CCM na kuichagua iendelee kuongoza, kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo,” alisema.

Tuesday, 12 January 2016

Lugha za kibaguzi, Uvaaji wa Sare za Chama Kwenye Shughuli za Kitaifa, Mambo Haya Yawe "Criminalized

CCM kuomba radhi,pamoja na watu mbalimbali kuendelea kukemea kitendo kilichotokea Zanzibar leo hii kwenye sherehe za Mapinduzi,nafikiri haya yote hayatoshi na wala hayatasaidi kitu na kwahivyo tunapaswa kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana na matukio ya aina hii katika siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu,wakati umefika tuwe na sheria,tena sheria kali, itakayozuia watu kuvaa sare za vyama vya siasa katika shughuli au matukio ya kitaifa.

Vile vile tunapaswa kuwa na sheria itakayokataza au itakayopiga marufuku kauli,vitendo na aina yoyote ya matukio ya kibaguzi au yenye mwelekeo wowote ule wa kibaguzi. Ubaguzi huu uwe wa rangi,dini au kabila.

Hili ni wazo tu ila naamini kuna wataalamu wa sheria wanaoweza kulifanyika kazi wazo hili na kuliboresha zaidi.

Wabunge mnao uwezo pia wa kupeleka hoja binafsi Bungeni kuhusu swala hili na si kuisubiri serikali tu ambayo nayo inaweza isilifanyie kazi wazo hili au ikachukua muda mrefu kulitekeleza.

Tujifunze kutokana na makosa na tuchukue tahadhari pia

Monday, 11 January 2016

Maalim Seif Sharif Hamad Kupasua JIPU Leo

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif  Hamad, leo  anatarajia kufichua siri ya mazungumzo ya kusaka suluhu, baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kufutwa mwaka jana.

Maalim Seif,  anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari  leo saa tano asubuhi kueleza hatima ya mazungumzo ya kisiasa ya kutafuta mwafaka Zanzibar

“Maalim Seif kesho (leo), atazungumza na wahariri na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano Zanzibar,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana.

Seif anachukua uamuzi huo wakati hali ya kisiasa visiwani humo ikizidi kuwa ngumu kwa pande zote, licha ya Rais Dk. John Magufuli kuahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Maalim Seif anajitokeza leo, wakati wiki iliyopita Rais Magufuli  alikutana na  viongozi wastaafu, ambao kwa pamoja walizungumza mambo mazito ya kitaifa pamoja na kutakiana heri ya mwaka mpya.

Wiki iliyopita Rais Dk. Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye alimhakikishia kumpa ushirikiano atakapohitajika kufanya hivyo.

Katika kumhakikishia kuwa yuko tayari kufanyakazi atakayomtuma, taarifa za ndani zinaeleza kuwa moja ya jambo kubwa ambalo Mkapa anaweza kulisimamia ni suala la kusaka suluhu ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Mkapa alisema lengo la mkutano huo ni kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa dhamana aliyopewa na Watanzania na kumtakia heri ya mwaka mpya.

Mkapa alimhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote na kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Licha ya Mkapa, Rais Magufuli pia alikutana na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, ambaye alikabidhi baadhi ya nyaraka kwa Rais Magufuli.

Kikwete alikabidhiwa nyaraka hizo zinazohusiana na mgogoro huo na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, Novemba 4, mwaka jana.

Inaelezwa kuwa Maalim Seif alikabidhi nyaraka mbalimbali, zikiwamo fomu za matokeo ya Uchaguzi  Mkuu kwa vituo vyote vya Zanzibar

Friday, 8 January 2016

habari zilizopo kwenye magaazeti ya leo

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 9, Ikiwemo Jide na Namless Wazua Gumzo Picha yao ya Mahaba yatua Kwa Gadner


Saturday, 31 October 2015

Profesa Kitila: Edward Lowassa na Ukawa Kubalini Yaishe..Kubalini Dk Magufuli Ndio Rais Wenu

Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.

Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.

Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea  nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang’anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.

Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.

 “Hivyo Lowassa na  wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali  kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye  jukumu la  kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.”

Aliongeza: “Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.”

Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku  CCM ikiwa na viti 188.

“Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,”alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;

“...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano. Wahakikishe wanashirikiana  na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi. Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.”