Thursday, 20 August 2015

Bulaya Hakuwa na Mpango wa Kuhama CCM ila…

Ester Bulaya Hakuwa na Mpango wa Kuhama CCM ila….

Najua nina watu wangu wanaopenda stori za siasa sasa stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia CCM Ester Bulaya pamoja anaonekana kwenye headlines mpya za Chadema baada ya kuhamia chama hicho anasema hakutegemea kuhama chama cha Mapinduzi (CCM).

Kuhama inatokea na mazingira lakini mimi sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuhamia Chadema lakini mienendo, tabia, future  ya kuwatumikia wananchi ilikuwa imepotea mimi nimekulia CCM na am proud for that  wamenilea lakini walinilea kwenye misingi ya uwazi na ukweli kile walichonifunza nikitaka kukitumia hawataki sasa kama kuna wengine kile nilichofundishwa huku wao wanakiaminia kutoka moyoni na midomo mwao niende kujiunga nao lakini wote tukiwa na ndoto za kuwatumikia wananchi’ -Ester Bulaya


Unajua kuna tofauti ya utumishi na mtu kufikiri utumishi ni cheo wanaofikiri ubunge ni cheo ni wale ambao hawatimizi wajibu wao wanataka ubunge kutaka madaraka Fulani, mimi ni mtumishi naenda kuwatumikia wananchi mabosi wangu ni wananchi ukiwa unadhani ya kwamba ubunge ni cheo utavimba kichwa na utashindwa kutimiza wajibu wako, bunge bosi wake ni wananchi‘ – Ester Bulaya.

0 comments:

Post a Comment