Wednesday 19 August 2015

CHELSEA WAIPIKU MAN UTD KUMNASA PEDRO


Chelsea wamefikia makubaliano na Barcelona kumsajili winga Pedro kwa pauni milioni 21. Mchezaji huyo, 28, ambaye alikuwa akisakwa na Manchester United, anasafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain, amepachika mabao 99 katika mechi 326 tangu alipoanza kucheza mwaka 2008. Atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea ndani ya wiki moja, kufuatia kuwasili kwa beki wa kimataifa wa Ghana Abdul Baba Rahman.

0 comments:

Post a Comment