Saturday, 1 August 2015

HUYU MSANII KUMBE DOMO ZEGE,AOMBA ATONGOZEWE WASTARA AMUOE,MCHEKI MWENYEWE

KUTOKANA na ugumu wa masharti aliyopewa na mwigizaji Wastara Juma juu ya kumuoa, msanii Bond Suleiman ‘Bond’ ameomba msaada kwa watu wa karibu hususan upande wa Wastara kumsaidia kumuweka sawa ili atimize lengo lake la kumuoa.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Bond alisema Wastara ni mwanamke mwenye kila sifa ya kuwa mke, hivyo endapo atamkosa litakuwa ni pigo kubwa maishani mwake.
“Jamani, amenipa masharti magumu sana, ni mwanamke thabiti ambaye nisingependa kumkosa, najaribu kuwatumia watu wetu wa karibu kumuweka sawa, maana ana kila sifa za kuitwa mke, nimekaa naye muda mrefu kama meneja wake, nimegundua mambo mengi sana, nahitaji msaada jamani,” alisema Bond

0 comments:

Post a Comment