Sunday, 23 August 2015

Lulu Michael Amponda Husna Maulid kuwa anamuibia...........soma hapa

STAA mdogo kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameonekana kumrushia vijembe hasimu wake mkubwa mlimbwende Husna Maulid kwa kile alichodai kuwa anamuibia maelezo yake ya picha (caption) kwenye mtandao wake wa Instagram.

Staa huyo ambaye hakumtaja Husna moja kwa moja, alisema kwa sababu amekuwa akiweka maelezo ya picha katika mtandao na mtu kuyaiba kama yalivyo na kuweka katika picha zake, ameamua kutoa onyo ili asiibiwe.

“Naweka caption lakini ina hati miliki, wewe unayechukua na kuhamishia kwako, tafadhali.” Aliandika Lulu mtandaoni ambapo alipoulizwa na mwandishi wetu kama alimtupia vijembe Husna, alisema:

“Jamani sijataja jina la mtu yoyote lakini kama kuna ambaye anajihisi basi ndio huyohuyo.”

Husna amekuwa akikopi maneno ambayo Lulu anayaweka katika kurasa zake kama: “You can copy my things but you can’t be me.” Husna naye anaandika hivyohivyo.

Wawili hao waliwahi kuwa marafiki kisha kutofautiana wakituhumiana kuibiana bwana

0 comments:

Post a Comment