Pakistan hii leo imemnyonga kijana Shafqat Hussain, mtuhumiwa wa mauaji ya kijana wa miaka saba yaliyofanyika mnamo mwaka 2004, licha ya malalamiko kutoka mashirika ya kutetea haki za binadamu yanayosema aliteswa ili kukiri alifanya mauaji hayo na alikuwa hajafikisha umri wa kuwa mtu mzima wakati mauaji hayo yalipotokea. Wataalamu wa kutetea haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa walikuwa wameelezea mashaka yao kuwa kesi dhidi ya Hussain haikuwa imetimiza viwango vya kimataifa na kuitaka Pakistan kutokumnyonga bila ya kuchunguza kikamilifu madai kuwa aliteswa kukiri kuua na kuwa alikuwa na miaka 15 mauaji hayo yalipotokea. Licha ya wito huo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, Hussain alinyongwa leo asubuhi katika jela moja iliyoko Karachi. Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelaani kunyongwa kwa kijana huyo
Tuesday, 4 August 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment