Monday, 17 August 2015

Penny Agoma Kuulizwa Kuhusu Mtoto wa Diamond Platnumz na Zari ..Kisa Hichi Hapa


Yamekuwa hayo? Aliyewahi kuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mwingilwa `DVJ Penny’ amegoma kuulizwa chochote kuhusu kitendo cha zilipendwa wake huyo kupata mtoto wakati yeye alidaiwa kukataa kumzalia.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Penny alifunguka kwamba, haoni kama kuna sababu ya kumzungumzia Diamond na mtoto wake (Tiffah) kwani walishaachana zaidi ya miaka miwili sasa.

Jamani, huyo mtu kwa sasa hanihusu na sioni kama kuna sababu ya kumuongelea mtoto wake, anayepaswa kuulizwa mambo ya Diamond ni Zari, kwa hilo mnisamehe (no comments), nikiulizwa niulizwe mambo yangu tu,” alisema Penny

0 comments:

Post a Comment