Edward Lowassa amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Dkt. John Pombe Magufuli amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia TLP, Macmillan Lyimo amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia ADC, Chief Lutasola Yemba amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia Chama cha UMMA, Hashim Rungwe amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia UPDP Fahmi Nassoro Dovutwa amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, Bi. Anna Elisha Mghwira amerudisha fomu ya kugombea urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Wagombea wengine kwa ufupi ni;
CHAUMA Rungwe amethibitishwa na Jaji tayari
John Dustan Chipaka kaingia ofisi za NEC na yeye,
chama cha NRA Janken Kasambala na mgombea mwenza Samai Abdulla wamewasili tayari wamethibitishwa na jaji
CCK wameshindwa kukidhi vigezo na masharti ya Tume, wenyewe kupitia kwa DKt. Malisa wamesema "Tumefungua shitaka mahakamani hivyo nategemea tume isitishe kwanza mchakato"
Chipaka wa TADEA nae akataliwa na tume kwa kuwa hajakidhi vigezo
Mch. Mtikila akishuka kwenye bajaji na fomu zake
Mch. Mtikila wa DP kakataliwa kwani hakukidhi vigezo. Alienda kuapa bila mgombea mwenza hivyo hakuapishwa.NEC yasema Ikifika saa kumi watafunga zoezi hilo, Mch. MTIKILA amerejea eneo la NEC na kuambiwa hajakidhi Vigezo, Yeye kasema Kukosa kugombea Urais hakutanizua kwenda Mbinguni.
Jumla ya Vyama nane na Wagombea wao, wamefanikiwa kurudisha fomu na wameidhinishwa na Tume ya Uchaguzi na wanaweza kuanza kampeni muda wowote kwa kuzingatia maadili na masharti ya tume ya kuendesha zoezi la kampeni.
Vyama vilivyo fanikiwa kuthibishwa na kukidhi vigezo ni;
UPDP
CHADEMA
CCM
TLP
ADC
ACT
CHAUMA
NRA
Vyama ambavyo havikukidhi vigezo ni;
TADEA
CCK
AFP- Mgombea hakuonekana kabisa wala fomu hajikurudishwa.
DP
0 comments:
Post a Comment