Thursday, 29 October 2015

wananchi wa china walegezewa mashart,sasa waruhusiwa kuzaa watoto wawili tu.


Mwanamke UchinaImage copyrightAFP
Image captionFamilia sasa zitaruhusiwa kuwa na watoto wawili
Uchina imeamua kusitisha sera yake iliyodumu miaka mingi ya kuzitaka familia kuwa na mtoto mmoja pekee, shirika la habari la Xinhua limeripoti.
Familia sasa zitaruhusiwa kuwa na watoto wawili, shirika hilo linalomilikiwa na serikali limesema, likinukuu taarifa kutoka kwa chama tawala cha Communist Party.
Sera hiyo tata ilianza kutekelezwa mwaka 1979, kupunguza ongezeko la watu nchini humo.
Hata hivyo, kumekuwepo na wasiwasi kutokana na kuwepo sehemu kubwa sana ya raia wazee kwa umri.
Sera hiyo ya kuzaa mtoto mmoja pekee inakadiriwa kuzuia watoto 400 milioni kuzaliwa tangu ianze kutekelezwa.
Waliokiuka sera hiyo waliadhibiwa, baadhi wakitozwa faini na kufutwa kazi na hata kulazimishwa kutoa mimba

0 comments:

Post a Comment