Monday 8 February 2016

Mimba ya Wema, Idriss Sultan Apachikwa Jina la Dk. Mwaka Baada ya Wengi Kushindwa Kumpa Ujauzito Wema

MIMBA ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu inazidi kuzua
ya kuzua kila kukicha baada ya hivi karibuni, Mshindi wa Big
Brother Africa Hot Shots 2015, Idriss Sultan ambaye
anajigamba kuwa ndiye mwenye ujauzito huo kupachikwa jina
la Dk. Mwaka.
Idriss amepewa jina hilo kwa vile Tabibu wa Tiba Mbadala
Tanzania, Juma Mwaka Juma JJ Mwaka au ‘Dk. Mwaka’
amekuwa akisifika kwa kuwatibu wanawake wenye matatizo
ya kutoshika mimba.
Mitandao mbalimbali ya kijamii wiki iliyopita ilimwita Idriss ni
Dk. Mwaka huku ikimsifia kuwa, wameshindwa wanaume
wengi, akiwemo Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
aliyewahi kuwa mpenzi wa Wema lakini yeye ameweza kumpa
furaha mrembo huyo kwa kumpachika ujauzito.
“Kweli wewe Idriss ni Dk. Mwaka. Maana Mwaka amekuwa
akiwasaidia wanawake kupata watoto. Wema ametoka na
wanaume kibao, lakini wewe dogo umeweza, big up!”
ulisomeka mtandao mmoja.
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Mwaka kwa njia ya simu ili
kumuuliza amelichukuliaje tukio la Idriss kuitwa kwa jina lake.
“Pengine uwezo wangu wa kazi umesababishwa aitwe hivyo.
Lakini mimi bado nabaki kuwa Dk. Mwaka orijino na kazi
yangu inajulikana,” alisema Dk. Mwaka.
Idriss hakupatikana hewani juzi kuzungumzia ishu hiyo lakini
kwa nyakati tofauti amewahi kucheka tu kwa watu kumwita
jina hilo.


0 comments:

Post a Comment