Tuesday 23 February 2016

Mkwanja wa dili la Voda ni ‘fifty fifty’ kati ya Diamond na Zari?

kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania.
Dili hilo limemfanya muimbaji huyo wa ‘Make Me
Sing’ aonekane kwenye matangazo ya TV, yale ya
barabarani, kwenye magezeti na vipeperushi vingine
pamoja na kusikika kwenye matangazo ya redio.
Kwenye tangazo la TV, si Diamond pekee
anayeonekana, bali familia yake nzima – wapo
mpenzi wake Zari, mwanae Tiffah na mama yake.
Lakini pia kuna tangazo moja la redio ambalo Zari
anasikika akiwemo pamoja na Diamond na Mpoki.
Yeye mwenyewe Dangote alidai kuwa familia yake
nzima ni brand na hilo halina ubishi. Lakini huenda
Zari akawa anamega kipande kikubwa pia cha keki
hiyo iliyotokana na mkataba wa Vodacom. Si jambo la
kushangaza kwakuwa Mganda huyo sasa ni ubavu wa
kushoto wa staa huyo na hakuna anayebisha kuwa
mrembo huyo amekuwa akipush zaidi kampeni ya
Ongea Deilee kwenye akaunti yake ya Instagram.
Lakini kibiashara, tunajua kuwa hata kama Zari ni
mpenzi wake na Diamond mwenye ubalozi huo, na
kwa ukubwa alionao, hawezi kupiga promo tu
kwasababu anamsaidia mume wake. Yaani kwa
mfano haijawahi kutokea Jay Z akimsaidia Beyonce
kupromote kampeni za Pepsi kisa anamsaidia mke
wake.
It’s good to be famous.

Zari
Hassan
Kwasababu ni kila mmoja
anasimama kama brand
inayojitegemea. The same applies kwa
Zari na Diamond. Na hivyo kwakuwa
tunaona jinsi Mama Tiffah alivyo
mstari wa mbele kupush kampeni hiyo,
tunaanza kufikiria kuwa huenda
wawili hao wamekula pasu mkwanja
huo unaotokana na ubalozi wa
Diamond – fifty fifty!


0 comments:

Post a Comment