WATU wawili akiwamo askari mmoja
wamenusurika kifo baada ya kupigwa
risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni
majambazi, waliofanikiwa kupora mfuko
wa fedha unaosadikiwa kuwa na zaidi ya
shilingi milioni 30.
Tukio hilo, lilitokea jana mchana majira ya
8:30 katika Mtaaa wa Mlandege Mkoa wa
Mjini Magharibi, ambapo majambazi hao
walimvamia mmoja wa wafanya biashara
wa Mchele hapa nchini aliyetambulika
kwa jina la Salum Issa Suleiman (50),
Mkaazi wa Baghani Mjini Unguja ,,
ambaye walimpora mfuko wake wa fedha
hizo wakati akiwa njiani kuzipeleka benki.
Mfanyabiashara wakati akiwa njiani
alijikuta akizingirwa na mojaya gari ndogo
na kuanzakushambuliwa kwa risasi
ambazo zilimjeruhi sehemu zake za
miguuni na ghafla kuanguka na ndipo
majambazi hao walipowezakufanikiwa
kumpora fedha hizo.
Wakati tukio hilo likitokea mmoja wa
askari polisi wa Kituo cha Malindi Sajenti
Hija Hassan Hija, alijaribu kupambana
namabambazi hao, lakini alishindwa
kufanikiwa baada na yeye kujeruhiwa
sehemu ya mkononi na mguuni kutokana
kushambuliwa kwa risasi.
Wakizungumza na gazeti hili, waathirika
wa tukio hilo, Mfanya biashara Salum
alisema, wakati alipokuwa akielekea
maeneo ya Benki hiyo ndipo ilipotokea
gari ndogo mbele yake na kumnadia
mwizi na hapo ndipo walipompiga risasi
ya mguu wa kulia na kumnyang’anya
fedha hizo na kuondoka nazo .
Kwa upande wake askari Hija alisema,
alipofika maeneo hayo ndipo alipomkuta
Mfanyabiashara huyo akiwa katika
harakati za kujinasua na hali na ndipo
askari huyo alipokwenda kumuokoa lakini
na yeye alishambuliwa na majambazi hao
na kufanikiwa kuondoka na kitita hicho
cha fedha zamfanyabiashara huyo,,
Hata hivyo, majeruhi hao bado
wanaendelea kupata matibabu katika
Hospitali kuu ya Mnazi mmoja na hali zao
walieleza kuwa zinaendelea vizuri.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini
Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam,
alisema ni kweli tukio hilo limetokea na
aliyeporwa fedha hizo ni Mfanyabiashara
wa Mchele katika maeneo ya Bandarini
ambae alikuwa akielekea katika Benki ya
PBZ tawi la Mlandege.
Alisema mfanyabiashara huyo alikuwa na
fedha zenye thamani ya shilling milioni
30,6,00,000, ambazo ni mali ya tajiri
wake anafahamika kwa jina la Yussuf
Mohamed, ambazo alikuwa anakwenda
kuziweka katika Benki hiyo.
Hata hivyo, Kamanda Mkadam, alitoa wito
kwa Wananchi wakati wanapokwenda
kuweka pesa kuacha kwenda kwa miguu
na kuwatumia askari kwani askari wapo
kwa ajili yao ili kuimarisha usalama wa
raia.
Sajenti Hija Hassan Hija, alijaribu
kupambana na mabambazi hao, lakini
alishindwa kufanikiwa baada na yeye
kujeruhiwa sehemu ya mkononi na
mguuni kutokana kushambuliwa kwa
risasi.Akiwa katika hospitali ya Mnazi
mmoja akjipata huduma ya kwanza.
Sunday, 28 September 2014
ZanziNews at 4:16 PM Majambazi wapora milioni 30.6 wajeruhi Polisi, Mfanyabiashara
04:07
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment