Mwuguzi mmoja nchini Kenya amehukumiwa kifo
baada ya mwanamke aliyemsaidia kuavya
mimbia kufariki miaka mitano iliyopita.
Nchini Kenya kuavya mimba ni kinyume cha
sheria ingawa matabibu kadhaa huendesha
shughuli hizo kisiri kwa sababu mapato yake ni
makubwa.
Jackson Namunya Tali, mwenye umri wa miaka
41, amehukumiwa kifo na Jaji Nicholas Ombija
mjini Nairobi, baada ya kupatikana na kosa la
kusababisha kifo cha msichana Christine Atieno
katika kituo cha afya anachosimamia .
Kulingana na taarifa ya mashahidi, Msichana
Atieno alitunga mimba ambayo hakutarajia na
mnamo Julai , mwaka 2009, na kuamua kutafuta
msaada kwa Tali katika kituo chake cha afya
katika eneo la Gachie, viungani mwa jiji la Nairobi
ambapo alitaka kuavya mimba hio.
Jaji aliambiwa Kwamba licha ya jaribio la kuitoa
mimba hiyo haikutoka na badala yake mtoto
aliyekua tumboni alikufa, hali iliyosababisha
marehemu kuvuja damu nyingi.
Mshtakiwa alipogundua hali ilikua mbaya alianza
kumpa msichana huyo madawa za maumivu.
Kisha akampeleka katika hospitali ndogo ya
Kaunti ya Kiambu.
Jaji alimpata na hatia ya kusababisha kifo cha
mama na mtoto
Wahudumu wa afya katika hospitali ya Kiambu
walipendekeza mgonjwa kupelekwa kwa matibabu
maaluum katika hospitali ya nyingine ambapo
angepokea matibabu ya dharura kwani hali yake
ilikua mbaya.
Hata hivyo msichana huyo, ambaye wakati huu
wote alikuwa akivuja damu akiwa ndani ya gari la
mshtakiwa alifariki dunia na muuguzi
aliyemhudumiwa kulaumiwa kwa kifo hicho na
kushtakiwa.
Hii ndio hukumu kali zaidi kutolewa nchini Kenya
kuhusiana na kifo kutokana na kuavya mimba.
Nchini Kenya kutoa haikubaliwi ila ikiwa maisha
ya mama yako hatarini
Mjadala ya kuhalalisha uavyaji mimba umevutia
hisia kali nchini Kenya wanaounga wakisema
itasaidia afya ya uzazi huku wapinzani wakisema
ni mauaji ya kiumbe asiye na hatia.
Thursday, 25 September 2014
Ahukumiwa kifo Kenya kwa kuavya mimba
11:24
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment