Friday, 24 July 2015

MBEYA KIMENUKA!Hii ndio style mpya ya kuomba kura,apiga goti kama yuko kwenye maombi



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya Watia nia ya Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM wamelazimika kuomba kura kwa aina tofauti kwa wanachama wao.
Makada hao walilazimika kupiga magoti, kugalagala ardhini, kulazimisha kuulizwa maswali, ili mradi wapiga kura wawaonee huruma na kuwachagua.
Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini, walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.
Vituko hivyo vilileta bashasha na burudani ndani ya kata hiyo, na kuwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu kulazimika kusimama ili kwenda kumuinua Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa, Fatuma Kasenga, aliyekuwa anagalagala ardhini kuomba kura. Nini mtazamo wako

0 comments:

Post a Comment