Friday, 24 July 2015

MASTAA WAMLIZA KAJALA USIKU..AUMIZWA VIBAYA..SHUHUDIA HAPA

IMG-20150722-WA0001-001

Kajala Masanja akibugujikwa na machozi baada ya kufanyiwa sapraizi hiyo.
Machozi ya furaha! Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja juzikati alijikuta akiangua kilio baada ya kufanyiwa ‘sapraizi’ na mastaa wenzake katika siku yake ya kuzaliwa.
Tukio hilo lilichukua nafasi usiku wa Julai 22, mwaka huu nyumbani kwake Sinza Afrikasana jijini Dar ambapo akiwa hana hili wala lile, mastaa hao akiwemo Jacob Steven ‘JB’, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda, Leah Richard ‘Lamata’ na wengineo walifika nyumbani hapo mida ya saa 6 usiku kisha wakajibanza nje.
IMG-20150722-WA0003-001…Akimwagiwa ‘wine’.
Baada ya muda, Lamata aliyekuwa kwenye msafara huo aligonga mlango wa nyumba ya Kajala na kufunguliwa huku wakiendelea na mazungumzo, Lamata alinyanyuka na kwenda kuzima taa kisha ghafla likaingia kundi la mastaa kila mmoja akiwa ameshika mshumaa unaowaka na keki.
Tukio hilo lilimfanya Kajala apate mshituko na kitendo bila kuchelewa taa iliwashwa kisha mastaa hao wakaanza kumuimbia huku wakimmwagia vimiminika kama vile maji na ‘wine’.
Hali hiyo ilimfanya Kajala alie sana na kuwapa kazi mashosti zake kumtuliza na baadaye walisherehekea hadi asubuhi.
Akizungumzia tukio hilo, Kajala alisema kuwa, furaha aliyokuwa nayo siku hiyo ndiyo iliyomfanya alie kwani amebaini ana watu wengi wanaompenda licha ya kuwepo wachache wenye chuki zao binafsi.
“Kwa kweli sikuamini kile kilichotokea usiku ule ndiyo maana nililia kwa furaha, wenzangu wameonesha upendo wa hali ya juu kwangu,” alisema Kajala huku akifuta machozi. 

0 comments:

Post a Comment