Tuesday, 28 July 2015

Mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ahukumiwa kunyongwa,Habari kamili ingia hapa

Mahakama nchini Libya imemhukumu kifo mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi akiwa hayuko mahakamani. Saif al-Islam amehukumiwa kifo leo kwa kukandamiza maandamano ya amani wakati wa vuguvugu la umma nchini humo mwaka 2011 yaliyofikisha mwisho utawala wa baba yake.
Mahakama hiyo pia imemhukumu adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa wa utawala wa Gaddafi , Abdullah al-Senussi na waziri wake mkuu wa zamani Baghdadi al-Mahmoudi , katika kikao kilichotangazwa moja kwa moja katika televisheni.
Hukumu hiyo dhidi ya al-Islam ilipitishwa bila yeye kuwepo mahakamani. Tangu alipokamatwa mwaka 2011 na kundi la waasi wa zamani, amekuwa akishikiliwa katika jimbo la Zintan ambalo linaipinga serikali ya mjini Tripoli, ambayo inatambuliwa na jumuiya ya kimataifa

0 comments:

Post a Comment