Baada ya zoezi la kumpata Mgombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu kupitia chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) kuvunjika siku 6 zilizopita, hatimaye limefanyika tena jana huku likigubikwa na vurugu pamoja na rushwa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza waandishi wa habari waliohudhulia uchaguzi huo walifukuzwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho Red Briged, kwa kuhofia kuripotiwa katika vyombo vya habari, kwa mara nyingine vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikiendelea katika uchaguzi huo kama ilivyokuwa awali.
Vijana hao walieleza kuwa walikuwa wakitekeleza agizo la Kiongonzi wao Kamanda wa Red Briged Kanda ya ziwa Esau Bwile, ambaye aliwataka kuwatoa nje ya ukumbi waandishi wa habari wote pamoja na askari polisi.
Vijana hao wa ulinzi walipoulizwa na waandishi wa habari sababu ya wao kutolewa nje, walieleza kuwa awali katika mkutano uliovinjika siku sita zilizopita waandishi hao waliripoti kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika mkutano wao hali iliyochafua sura ya chama chao.
“ tunaomba waandishi wa habari mtoke nje ya ukumbi…tumeagizwa na Mkuu wetu…amesema waandishi wa habari pamoja na askari polisi hawatakiwi ndani ya mkutano huu..sababu katika mkutano wa kwanza habari zenu zilichafua chama..mliripoti kuwepo kwa rushwa ingawa ilikuwa kweli lakini ilichafua chama” Alisema mmoja wa Red briged.
Aidha miongoni mwa waandishi wa habari ambaoa walifukuzwa katika mkutano huo wa uchaguzi ni mwandishi wa habari hii, Happy Severine (Nipashe), Faustine Fabian (Mwananchi) Berensi China (ITV) Paschal Michael (Chanel Ten) Costantine Mathias (Raia Tanzania).
Waandishi wa habari hao waliamua kutekeleza agizo hilo, ambapo awali kabla ya kutolewa nje walikuwa wakifuatiliwa baadhi ya wagombea walikuwa wakituhumiwa kwa mara nyingine kutoa rushwa.
Hata hivyo ilibainika kuwa mmoja wa wagombea alikuwa ameandaa vijana kutoka katika wilaya ya Meatu, wakiwemo Baadhi ya Red Briged kuanzisha vurugu ikiwa atashindwa huku wakionekana na mapanga, vurugu, pamoja na visu.
Baada ya kugundulika kwa vitendo hivyo ndani ya uchaguzi, ilibainika kuwa kilikuwa chanzo cha waandishi wa habari kutolewa nje ili wasiripoti kwa mara nyingine vitendo hivyo ili kuchafua chama.
“ sisi tuliitwa na viongonzi wa Chadema kuja katika uchaguzi huu..lakini tumeshangaa viongozi hao akiwemo katibu wa wilaya kutugeuka na kututoa nje…lakini tumebaini chanzo cha sisi kututoa nje” Alisema Mwandishi wa habari wa chanel ten
Hata hivyo kabla ya kufukuzwa kwa waandishi tayari taarifa na vielelezo vyote vya kuwepo kwa silaha ndani ya ukumbi kwa baadhi ya red Briged ,kulikuwa na vitendo vya rushwa na ndio maana waliamua kuwafukuza
Mbali na hali hiyo vijana hao wa ulinzi kutoka wilaya ya Bariadi walianza kugombana na vijana wa red briged kutoka wilayani Meatu, kwa madai kuwa wameingiliwa kikazi bila ya kupewa taarifa.
Vile vile baadhi ya wanawake wajumbe wa Bawacha waliulalamikia uongonzi wa Chama hicho kwa kuwafungia nje ya ukumbi ikiwa pamoja na kunyimwa chakula bila ya kutolewa sababu maalumu.
Aidha taarifa za matokeo ya uchaguzi huo hazikuweza kupatikana kutokana na matokeo kuchelewa kutolewa mpaka leo asubuhi, huku katibu wa chama hicho wilaya Suleman Ling’ondo akiomba radhi kufukuzwa kwa wandishi wa habari.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment