Mwigizaji mwenye jina kubwa ndani ya sanaa ya maigizo Bongo, Riyama Ally amekiri kutamani maisha ya ndoa huku akishikilia alichokisema ‘nasubiri wakati wa Mungu’.
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu hivi karibuni, msanii huyo mwenye sifa za kuvaa uhusika wa huzuni na kulia katika filamu nyingi, alisema akiwa mwanamke aliyekamilika, anahitaji kuwa na mume wake katika ndoa takatifu lakini akaweka wazi kuwa kwa sasa ana mchumba ambaye anamuomba Mungu usiku na mchana ili awe mumewe.
“Kila mtu aliyekamilika anahitaji maisha ya ndoa, hakuna kitu chenye heshima katika maisha ya binadamu kama kuwa na ndoa na kuishi kwa amani, lakini kila kitu hupangwa na Mungu. Kiukweli kabisa natamani sana ndoa, nina mchumba ambaye namuomba Mungu amfanye kuwa mume wangu,” alisema Ri
0 comments:
Post a Comment