Tuesday 25 August 2015

HAMHREY POLEPOLENAE YAMEMKUTA,ATEKWA NA MAJAMBAZI NA KUNYANAGANYWA KILA KITU

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Hamphrey Polepole ametekwa na majamabzi Jijini Dar Es salam ambapo taarifa zimesema kuwa ametekwa na kunyanganywa kila kitu.
Taarifa zinasema alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake,Mbezi Beach, Dar.
Polisi walifika haraka eneo la tukio. Hakuna madhara yaliyoripotiwa, pia hakuna aliyekamatwa kuhusishwa na tukio hilo.
Pole pole ambaye ni mwanachama wa CCM alikuwa mwiba kwa serikali na chama hicho akiipinga juu ya kufinyangwa kwa baadhi ya vipengele vya katiba mpya chini ya CCM lakini katika siku za hivi karibuni amebadilika na kuanza kushambulia upande wa upinzani juu ya kupata mgombea urais ambaye ni Edward Lowassa hali iliyomwongezea marafiki na maadui

0 comments:

Post a Comment