Wednesday, 13 January 2016

JE Umewahi Kusikia Tetesi Kuwa Mwigizaji Ray na Chuchu Hans Wamemwagana? Basi Chuchu Hans Kasema Haya

Chuchu Hans na Ray Mahabani
Msanii wa filamu nchini, Chuchu Hans amesema bado yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Vicent Kigosi aka Ray licha ya hivi karibuni baadhi ya watu kudai wawili hao hawapo tena pamoja.

Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV Jumanne hii, Chuchu alisema toka aanze kutoka kimapenzi na staa huyo mengi yamezushwa juu yake.

Sasa hivi haya mambo ya mitandao yanapotosha sana jamii na watu wanataka ufanye kile wanachotaka,” alisema. “Sijaachana Ray na wala hatuna mpango huo sema kuna baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wanataka tuishi maisha yao kitu ambacho hakiwezekani.

Pia Chuchu alisema madai ya kuachana na Ray yamekuja baada ya kufuta baadhi ya taarifa za mpenzi wake katika mtandao wa kijamii.
Chuchu Hans Katika Pozi

Sisi tulikuwa na utaratibu mimi nikipost kitu na Ray anapost kitu lakini baada ya kuacha watu wakajua si tumeachana lakini sisi tupo safi kabisa,” alisisitiza Chuchu.

Hata hivyo mwanadada huyo amewataka watu wa kwenye mitandao ya kijamii kuacha tabia za kumtukania wazazi wake pamoja na ndugu zake kwani wao hawahusiani na mambo yake binafsi

0 comments:

Post a Comment