Wednesday, 13 January 2016

NDOA ya Wastara na Mbunge wa CCM Nusura Itoe Uhai wa Bond Aliyekuwa Boyfriend wake

DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita siku chache tangu staa wa filamu, Wastara Juma kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge,  Zanzibar, Sadifa Juma aliyekuwa mpenzi wake, Bond Suleiman nusu afe, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.

Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa karibu wa kijana huyo ambaye pia ni muigizaji (jina linahifadhiwa) alisema siku moja kabla ya ndoa ya Wastara, Bond alitaka kujiua kwa kunywa sumu, lakini kaka yake aliyeingia chumbani kwake ghafla, akamuwahi kabla hajaibugia.

Ni Mungu tu Bond kuwa hai mpaka sasa, japokuwa hayupo vizuri ni kama amepaniki kutokana na Wastara kuolewa, maana bado anampenda, ungekuta sasa hivi tunaongea mengine, kwani alikuwa ameshaweka sumu tayari anywe, lakini alisahau kufunga mlango ikawa ndiyo salama yake baada ya kaka yake kuingia chumbani kwake akiwa anahitaji kuzungumza naye ndipo akakutana na ishu hiyo na kufanikiwa kumuokoa.

Ukweli hata sisi tumeumia sana Wastara kuolewa na mtu mwingine kwani tulikuwa tukimfahamu kwamba atakuja kufunga ndoa na Bond maana aliwahi kuletwa kutambulishwa kwa ndugu,” alisema ndugu huyo.

Mwaka 2015, Wastara na Bond wakilishana keki kwenye birthday

Gazeti hili lilimtafuta Bond ili kupata ukweli wa habari hizo, ambapo alikiri kuokolewa na kaka yake baada ya kutaka kunywa sumu kutokana na Wastara kuolewa.

Nilikuwa nimeshaandaa sumu kabisa na Wastara nilimuaga kwa njia ya meseji na hii ni baada ya kuniambia siku inayofuata anaolewa, ukweli nilimpenda na najuta maana mimi ndiyo nilifanya makosa na kumkosea sana, lakini siku niliyoamua kuachana na mambo ya ufuska na kuwa mtu wa sala muda wote, naye naona ndiyo akasema basi hanitaki tena.

“Nilijitahidi sana kumuomba msamaha lakini akanikatalia na kusema amempata atakayempa faraja ya moyo, namtakia maisha mema ya ndoa na nitamsubiri kama ndoa itavunjika nitamuoa maana mwenyewe wakati anasubiri kufunga ndoa (Alhamisi iliyopita) aliniambia kwamba anaogopa ndoa hiyo,” alisema.

0 comments:

Post a Comment