Tuesday, 12 January 2016

Lugha za kibaguzi, Uvaaji wa Sare za Chama Kwenye Shughuli za Kitaifa, Mambo Haya Yawe "Criminalized

CCM kuomba radhi,pamoja na watu mbalimbali kuendelea kukemea kitendo kilichotokea Zanzibar leo hii kwenye sherehe za Mapinduzi,nafikiri haya yote hayatoshi na wala hayatasaidi kitu na kwahivyo tunapaswa kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana na matukio ya aina hii katika siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu,wakati umefika tuwe na sheria,tena sheria kali, itakayozuia watu kuvaa sare za vyama vya siasa katika shughuli au matukio ya kitaifa.

Vile vile tunapaswa kuwa na sheria itakayokataza au itakayopiga marufuku kauli,vitendo na aina yoyote ya matukio ya kibaguzi au yenye mwelekeo wowote ule wa kibaguzi. Ubaguzi huu uwe wa rangi,dini au kabila.

Hili ni wazo tu ila naamini kuna wataalamu wa sheria wanaoweza kulifanyika kazi wazo hili na kuliboresha zaidi.

Wabunge mnao uwezo pia wa kupeleka hoja binafsi Bungeni kuhusu swala hili na si kuisubiri serikali tu ambayo nayo inaweza isilifanyie kazi wazo hili au ikachukua muda mrefu kulitekeleza.

Tujifunze kutokana na makosa na tuchukue tahadhari pia

0 comments:

Post a Comment