Tuesday, 12 January 2016

Mazito Yaibuka Ndoa Mpya ya Wastara...Ndugu wa Marehemu Sajuki Waangua Kilio

HAYA ni mazito! Nyuma ya shughuli ya kuolewa kwa staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliyofungwa Alhamisi iliyopita, kuna matukio ya kustaajabisha ambayo Ijumaa Wikienda limeyabaini.

Ndoa hiyo iliyofungwa kimyakimya, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa mwigizaji huyo, Tabata-Barakuda, jijini Dar ambapo ilihudhuriwa na watu wachache tofauti na ilivyotarajiwa kutokana na umaarufu wa wanandoa hao.

NDOA ILIFUNGWA KWA SIMU
Imebainika kuwa, awali ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa kumi jioni na baadaye kuelezwa ilisogezwa mbele hadi saa 12 jioni, hata hivyo haikufungwa muda huo baada ya bibi harusi kuchelewa kufika akitokea saluni alikoenda kupambwa na kulazimika shehe afungishe ndoa hiyo kwenye simu wakati Wastara akiwa kwenye foleni barabarani.

BWANA HARUSI AGOMA KUPIGWA PICHA
Imeelezwa kuwa, baada ya bwana harusi kutinga na wapambe wake alitoa onyo kali huku likisisitizwa na wapambe wake kuwa hairuhusiwi kupiga picha na kutuma kwenye mtandao wowote wa kijamii kwa vile ndoa hiyo ilikuwa ya siri.

AGOMA KUMFUNUA BIBI HARUSI
Katika hali ya kushangaza, baada ya bibi harusi kuwasili aliingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya kumsubiri mumewe na hata alipoingia ndani, shehe alimuomba amfunue mkewe ili kumhakikisha kama ndiye yeye kitu ambacho alikipinga na kudai hakuwa na shaka naye na kuomba waendelee na kitu kingine.

WASTARA ASHINDWA KUPATA MSOSI
Jambo lingine ambalo lilizua minong’ono ni Wastara kushindwa kupata muda wa kula chakula ambacho kiliandaliwa kwa sababu baada ya kumaliza kupiga picha za familia na kushikana mkono na mumewe, mumewe alimtaka waondoke huku akimwambia dereva wao awashe gari.

WADOGO WA SAJUKI WALIA
Katika hali ambayo haikuweza kufahamika mara moja, wadogo wa aliyekuwa mumewe wa pili wa Wastara, merehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Mohamed Kilowoko na Njegere Kilowoko waliangulia kilio kwa kile walichodai walikuwa na huzuni na furaha.

0 comments:

Post a Comment