Ingawa Shilole tayari amefunika tattoo aliyochora kifuani yenye jina la ex wake Nuh, kwa kuongeza mchoro wa ua juu yake baada ya wawili hao kuachana, Nuh Mziwanda amesema yeye bado hajaamua kufuta tattoo zake.
Nuh ambaye alichora tattoo mbili, moja ikiwa na jina la Shishi Baby na nyingine ikiwa na sura ya Shishi amesema kuwa endapo atapata mwanamke wa kuziba pengo la Shishi ndio atafuta tattoo hizo.
“Mimi sijatoa hii tattoo sababu sijapata bado mwanamke ambaye anayeweza ku-cover nafasi ya yule mwanamke, nikipata mwanamke ambaye ataweza kucover nafasi ya yule mwanamke, akinishawishi kweli kuona anatabia ambazo mimi nazitaka basi…” alisema Nuh kupitia AYO TV.
Nuh aliendelea kueleza sababu za yeye kuchora tattoo za Shishi kwenye mwili wake.
“of-course yule mwanamke mimi nilimpenda kweli na mimi ndio nilianza kuchora tattoo kwake yeye so I was real, nilichora tattoo kwa mapenzi sikuchora kwasababu ya. Unajua ukichora tattoo kwasababu ya inamaanisha moyoni unakuwa unaumia unatamani ile tattoo uitoe ndio maana hata yeye (Shishi) aliweza kuibadilisha ikawa ua. “.
Chanzo cha ugomvi kati ya Shilole na Nuh Mziwanda kilichopelekea penzi lao kuvunjika kimeendelea kubaki kuwa siri yao, kutokana na wote kutotaka kukisema licha ya Shishi kuweka wazi kuwa Nuh ndiye mkosaji.
“Sipaswi kusema kitu gani kimetokea au kipi ambacho kimefanya mimi na bibie tuweze kutengana kwasababu ni maisha. Katika maisha kuna kupata na kukosa kwahiyo unaweza ukampata mtu na ukamkosa mtu, so kuachana ni kitendo cha kawaida tu ambacho kipo katika maisha yetu ya kila siku.” Alieleza NUh.
“Kama yeye anasema mimi ndio nimemkosea its okay all in all najua Mungu yupo na anatuangalia sisi binadamu tunafanya nini, mimi mama yangu kanifundisha kaniambia mtoto wa kiume hutakiwi kuongea, mtoto wa kiume unasifiwa kazi, kwahiyo kama yeye anasema mimi ndo nimemkosea its okay ila moyo wake unajua kitu gani kinaendelea.” Alisema Nuh Mziwanda ambaye amekuwa kwenye uhusiano na Shishi kwa miaka mitatu.
Monday, 11 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment