Rais wa Marekani Barack Obama ametumia
hotuba yake katika kikao cha baraza la Umoja
wa Mataifa kuomba ushirikiano wa mataifa
mengine katika vita dhidi ya kile alichokitaja
kama mtandao wa chuki, mauaji na uhasama.
Matamshi ya Obama yalilenga kundi la wapiganaji
wa kiisilamu la Islamic State nchini Syria.
Rais Obama, amesema kuwa Marekani itatumia
nguvu kwa ushirikiano na washirika wake na
kuwafunza pamoja na kuwapa silaha wanajeshi
wanaopambana na I-S , wakati ufadhili wa kundi
hilo ukiangamizwa.
Rais Obama atakuwa mwenyekiti wa mkutano wa
baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
utakaofanyika baadaye mwaka 2000.
Alisema kuwa watafikia azimio ambalo litaeleza
jukulu la kila nchi katika kupambana na uenezwaji
wa itikadi kali ambao unaambatana na ghasia.
Awali, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-
moon, alizungumzia unyama unaotendwa na
kundi la Islamic State na alichokiita mauaji
yanayoendelezwa na wapiganaji wa Boko Haram.
Wapiganaji wa Islamic State
Wakati huohuo, ndege za kivita za Marekani
zimefanya mashambulizi ya angani dhidi ya
wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq na Syria,
na kuharibu magari na maeneo yenye silaha.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jeshi la Marekani.
Magari manane ya IS yaliharibiwa karibu na eneo
la Abu Kamal upande wa mpaka wa Syria na Iraq
pamoja na maeneo mengine mawili ya Deir al-
Zour Mashariki mwa Syria.
Nchini Iraq, mashambulizi yalifanywa dhidi ya IS
Magharibi mwa Baghadad na Kusini Mashariki
mwa Irbil karibu na eneo la Kikurdi.
Wednesday, 24 September 2014
Obama aomba ushirikiano dhidi ya IS
21:53
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment