Batuli Amshukia Kitale Kwa Kuvujisha Picha Hizi Mtandaoni
Staa wa mrembo wa Bongo Movie, Batuli ameonyesha kuchukizwa kwake kwa kitendo cha staa mwenzake, Kitale kuvujisha picha hizi akiwa faragha na mwigizaji chipukizi, Stanbakora ikiwa ni kati ya moja ya kipande cha kazi yao mpya, kwa madai kuwa anaipa ‘promo’.
Kupitia ukurasa wake mtandao Batuli ameeleza kuwa Kitale alimpa picha hizo Mateja ambaye ndiye aliezisambaza kwenye mtandao wa Instagram.
“Kwanza mniwie radhi Watanzania mnachokiona na kinachoelezewa ni vitu viwili tofauti mwenye akili timamu anapata jibu kamili. @mkudesimbaoriginal nikuulize hivi wakati unampa @matejamusa picha ulimwambia ni za nini!? hivi naweza kuwa faragha mbele ya camera!?
Hata kama unapromote movie hii sio kiivyo kama kupromote kitu ndio hivi basi fani yetu imejaa mazumbukuku, hii ni scene iliyopo kwenye movie sioni sababu ya kunichafua kijinga hivi, kizuri kinajiuza @mkudesimbaoriginal kuandika shit sio njia sahihi ya kupromote kazi yako”- Batuli aliandika.
0 comments:
Post a Comment