Saturday, 1 August 2015

HII NDIO LIST YA KINGWENDU YA WASANII ANAO WAKUBALI TANZANIA

Mkali wa kitambo kwenye sanaa ya vichekesho Kingwendu amepata nafasi ya kuongea na millardayo.com na kukubali kushare nasi mambo kadhaa ikiwemo mastaa wa Tanzania anaowakubali na sababu za kuwakubali.
List ya wakali wake kaanza nayo kwenye muziki  wa Bongo Fleva ambapo amesema ‘Kwa muziki kwanza namtaka Diamond namkubali pia Alikiba namkubali pia Rich Mavoko halafu kuna huyu dogo amedrop sasa hivi Tid nilikuwa naye Burundi miezi 3 tunapiga nae kazi namkubali sana wa tano ni huyu dogo amechipukia hivi karibun anaitwa Dimpoz(Ommy Dimpoz)huyu mtoto nae mbaya sana’
Upande wa maigizo Kingwendu amesema ‘Upande wa movie nawakubali zaidi kwenye naanza na Mzee Majuto,halafu kuna Joti halafu kuna huyu Jb safi sana anajitahidi sana katika maisha halafu kuna dogo anaitwa Hemed ni Handsome Boy yule mtoto nae balaa hao niliokutajia nawakubali kwa sababu ni watu wa kazi hao.

0 comments:

Post a Comment