Friday, 28 August 2015

Kipindupindu cha piga hodi Nyumbani Kwa Wema Sepetu


Mrembo Wema Sepetu
Taarifa za ugonjwa wa kipindupindu zimebadili mfumo wa maisha ya watu wengi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maeneo wanayoishi ni masafi lakini nyumbani kwa msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Kijitonyama jijini Dar hali ni tofauti.

Mwandishi wetu akiwa kwenye mishemishe zake hivi karibuni, alikuta uchafu mwingi nje ya geti la nyumba ya msanii huyo hali iliyoelezewa na majirani kuwa ni kuukaribisha ugonjwa huo hatari.
Uchafu huo ulikuwa umezagaa katika eneo hilo ukiwa kwenye mifuko ya plastiki na kutoa harufu mbaya huku kunguru na paka wakipata pa kuponea njaa.

Akizungumza na Ijumaa mmoja wa majirani wa Wema alisema kuwa, ni kweli uchafu huo haukustahili kuwepo katika eneo hilo hasa katika kipindi hiki lakini akadai huenda uliwekwa na watu.
“Ni kweli kwa hatari ya ugonjwa huu wa kipindupindu uliolipuka, uchafu kama huu si sahihi kuwepo hapa lakini ninachohisi labda wale wavuta unga wanaozoa taka wamemuwekea usiku,” alidai jirani huyo.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuzungumza na Wema lakini geti lake lilipogongwa halikufunguliwa na alipopigiwa simu hakupokea

0 comments:

Post a Comment