Wednesday, 1 October 2014

Arsenal yapiga mtu,liverpool yaangukiavpua


Mechi za klabu bingwa barani Ulaya iliendelea
usiku wa kuamkia Alhamis wakati timu kadhaa
ziliposhuka dimbani.
Vijana wa mzee Wenger, Arsenal, ulikuwa usiku
wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1
dhidi ya Galatasaray ya Uturuki, huku mchezaji
mpya wa timu hiyo Danny 'Electric' Welbeck
akiondoka na mpira baada ya kuzifumania nyavu
za wapinzani wao mara tatu, moja likifungwa na
Allexis Sanchez.
Katika mchezo huo Arsenal walimaliza pungufu
baada ya kipa wao Wojciech Szczeny kutolewa
kwa kadi nyekundu katika dakika ya 60 ya
mchezo.
Wakati hayo yakijiri vijogoo wa Anfield Liverpool
walikuwa ugenini huko Uswis na kujikuta
wakiangukia pua baada ya kufungwa bao 1-0 na
FC Basel.
Mabingwa watetezi Real Madrid waliendeleza
wimbi la ushindi kwa kuisasambua Ludogorets
Razgrad ya Bulgaria kwa jumla ya mabao 2-1.
Christiano Ronaldo na Kareem Benzema ndio
waliopeleka ushindi kwa vijana hao wa Benabeu.
Kwingineko Atletico Madrid waliialika Juventus ya
Italia, hadi mwisho wa mchezo Atletico ikaibuka
na ushindi wa goli 1-0.
Borusia Dotmund wakaikaanga Anderlecht kwa
mabao 3-0. Bayern Liverkusen wakaiangamiza
Benfica kwa mabao 3-1, huku Malmo FF ya
Sweden wakawaduwaza Olympiakos ya Ugiriki
kwa mabao 2-0.

0 comments:

Post a Comment