Wednesday, 12 August 2015

Gazeti la Uhuru: Vijana waliomsindikiza Lowasa kuchukua fomu jana ni VIBAKA

Gazeti la Uhuru: Vijana waliomsindikiza Lowasa kuchukua fomu jana ni VIBAKA

Ni kitambo sana gazeti dada la chama Cha Mapinduzi limekua likinanga Harakati za vyama pinzani. Yote tisa kumi ni ripoti zilizomo kwa gazeti hili tar 11/08/2015 siku moja baada ya MTETEMO WA UKAWA JIJINI DAR.

"Ati Kundi la vibaka latikisa Ukawa. " hao vibaka mliwaona wapi, hizo fedha walizolipwa mliziona kwa nani, na hizo Pombe walizokunywa mliwanywesha?

Mmeanza kukata mauno hata ngoma bado haijaanza kudunda? Mtachoka mapemaaa. Kama Gazeti ni la kimapinduzi wapeni watu habari zenuu, msiwapotoshe watu kwa vitu walivyovishuhudia.

Niwaulize kidogo.

Hiviii Wizi wa kura katika michakato ya majimboni si habari? Semeni hayo.

Na je Rushwa iliyoota mizizi katika Harakati za uteuzi si habari? Andikeni hiyo

0 comments:

Post a Comment