Rais wa Marekani Barack Obama amesema
Marekani itashambulia kundi linalojiitaa Islamic
state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima
kabisa makao ya kujificha .
Bw Obama amesema kushiriki kwa mataifa
kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo
kunaonyesha wazi hivyo si vita vya Marekani
pekee bali wao ni sehemu ya muungano wa
mataifa yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia
ISIL.
Pia amekiri kuwa mashambulio hayo yamelenga
pia wale aliowataja kuwa wanamgambo sugu wa
al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao
anasema wanalenga kuishambulia Marekani.
Nazo taarifa za jeshi la Marekani zasema
malengo ya mashambulio yaliyofanywa
yametimia.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa
wakifanya mauaji na utekaji nyara
Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa
kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema msemaji wa wizara ya mambo ya nje
wa Urusi Alexander Lukashevichy amesema
mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti
yazingatie sheria za kimataifa.
Kadhalika Obama, amesema kuwa kuhusika kwa
nchi za kiarabu katika vita dhidi ya wanamgambo
wa Islamic State nchini Syria ni dalili toshja kuwa
vita hivi sio vya Marekani pekee.
Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la
kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu,Jordan na Bahrain
zote zilituma ndege za kijeshiu katika opereshei
hiyo.
Tuesday, 23 September 2014
Obama aapa kuangamiza Islamic State
21:46
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment