Sunday, 9 August 2015

NUKUU YA ZITTO KABWE:WANASIASA TUSIWAFANYE WATANZANIA WAJINGA WASIO NA UWEZO WA KUTAFAKARI

NUKUU YA ZITTO KABWE
“Wanasiasa tusiwafanye watanzania ni wajinga wasio na uwezo wa kutafakari na pia hata kukumbuka kuwa jana tuliwaambia nini.
Haiingii kwenye akili za watu makini kuona Chama cha Upinzani kinampokea mtu ambaye kwa miaka nane viongozi wake wamezunguka nchi nzima kuutangazia na kuwaaminisha watanzania kuwa Edward Lowassa ni fisadi; kisha katika muda wa wiki moja viongozi hao hao wanajigeuza kuwa mahakama na kumsafisha na kumpa nafasi ya kugombea urais wa nchi kwa kuwaambia wananchi kuwa ati hakuwa fisadi bali ni mfumo wa CCM tu ndio uliokuwa unahusika!
Ni Viongozi wa chama hicho hicho waliopata kuituhumu ACT-Wazalendo kuwa imeusaliti upinzani kwa kufadhiliwa na Edward Lowassa katika uendeshaji wa ustawi wake na kwamba kilikuwa kinamwandalia makazi mapya mara atakapoihama CCM.
Namshukuru sana Mungu kuwa ameonyesha ameweka wazi mapema kuwa waliokuwa wanafadhiliwa na Lowassa kwa kipindi cha muda mrefu ni CHADEMA na wala sio ACT-Wazalendo."
Zitto Kabwe
Kiongozi Mkuu (ACT- Wazalendo)

0 comments:

Post a Comment