Wednesday, 29 July 2015

BAADA YA WEMA KUGONGA MWAMBA;Jacqueline Wolper nae kumfuata lowasa ndani ya UKAWA

Liwalo na liwe! Kinara wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameahidi kuambatana na waziri mkuu wa zamani ambaye ni Mbunge wa Monduli kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Ngoyai Lowassa kwenye safari yake ya kuhamia kwenye muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akizungumza  wikiendi iliyopita, Wolper alisema kwa mapenzi aliyonayo kwa Lowassa yupo tayari kwenda kokote hata kama siyo Ukawa.
“Mimi ni ‘Team Lowassa’, atakapohamia nami niko nyuma yake hata kama siyo Ukawa, nitamfuata, mimi na Lowassa ni damdam, hilo halina ubishi,” alisema Wolper.

0 comments:

Post a Comment