Monday, 17 September 2018

JINSI YA KUMFURAHISHA MKEO

Ili kusaidia familia za Kiislam na kueneza mafundisho ya Uislam katika kujenga familia, MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta, Canada, kimetayarisha ufupisho wa tafsiri ya vitabu viwili. Vitabu katika lugha ya kiarabu vilivyotungwa na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid. Mwanachuoni wa Kimisri, ambaye amemaliza masomo yake katika chuo cha Islamic University cha Madiyna An-Nabiwiyyah huko Saudi Arabia. Vitabu vyenyewe ni :
1.    Namna ya kumfurahisha Mkeo
2.    Namna ya kumfurahisha Mumeo
Hivi ni vitabu vizuri kabisa vya Kiarabu ambavyo tumeviona
katika somo hili. Vimekwenda mbali katika kuelezea, kuanzia
haki na wajibu mpaka adaab (tabia njema) na kwenda mbali
katika kutekeleza haki hizi katika maisha ya kila siku. Ufupisho ufuatao unamulika zaidi katika majukumu  ya nini kinaweza au kinachotakiwa kifanywe. Kila jambo lililotajwa na muandishi limeegemezwa katika ushahidi wa Qur-aan, Sunnah au matendo ya Maswahaba, bali ushahidi haukuwekwa katika tafsiri hii. Ifuatayo ni tafsiri ya kitabu cha kwanza.
Usisite kuituma kwa wengine au kuitoa kopi kwa njia nyoyote, ilimradi tu hutofanya mabadiliko yoyote, au kuongeza, au kupunguza bila ya ruhusa.
Ifuatayo ni sehemu ya KWANZA ya ufupisho wa kitabu “ How to make your wife happy” na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid.

1.    Mapokezi Mazuri
Baada ya kurudi kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisheni: 
·         Anza kwa maamkizi mazuri
·         Anza kwa Assalaamu 'Alaykum na tabasamu.
·         Salaam ni Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.
·         Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka baadae.



2.       Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha
·          Chagua maneno mema na jiepushe na maneno mabaya.
·          Shughulika nae unaposema au anaposema yeye
·         ·Sema kwa ufasaha na rejea maneno inapohitajika mpaka  afahamu/aelewe.
·          Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda, mfano Mpenzi wangu, honey (asali, tamtam),  (habibty),  swaaliha (mwanamke mwema), n.k



3.       Urafiki na maliwazo
·          Tumia muda kuzungumza nae
·          Mfikishie habari njema
·          Kumbuka kumbukumbu  zenu  nzuri za kuwa  pamoja. 


       
4.       Michezo na burudani 
·         Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya furaha
·         Chezeni na mshindane katika michezo na mambo mengine.    
·         Mchukue kuangalia aina za burudani zilizo halali.
·         Jiepushe na mambo ya haram katika kuchagua aina ya burdani.


5.                  Msaada katika kazi za nyumbani
              ·         Fanya kile ambayo wewe mwenyewe unaweza/ unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa anapokuwa mgonjwa au amechoka.
·         La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha wazi kuwa unathamini/unashukuru jitihada zake katika kazi.


6.                  Kushauriana (Shuura)


·          Hususan katika masuala ya familia
·          Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu kwako.
·         Kuyazingatia maoni yake kwa makini
·         Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa maoni yake iwapo yatakuwa ni bora zaidi.
·         Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.


7.                  Kutembelea wengine


·         Chagua watu wenye malezi mema wa kufanya mahusiano nao. Kuna malipo makubwa katika kuwatembelea jamaa na watu wacha Mungu. (Sio kuwatembelea kwa kupoteza wakati)
·         Kuwa muangalifu kuhakikisha tabia za Kiislamu wakati mnapowatembelea watu.
·         Usimlazimishe kuwatembelea wale ambao yeye hajisikii raha kuwa nao.


8.                  Muongozo wakati wa kusafiri


·         Muage vizuri na kumpa ushauri mwema
·         Mtake akuombee dua
·         Watake jamaa wacha Mungu na marafiki kuiangalia familia wakati wa kutokuwepo kwako.
·         Mpe pesa za kutosha kwa mahitaji anayoweza kuhitajia
·         Jaribu kuwa na mawasiliano nae ama kwa simu, e-mail (barua pepe), barua, n.k.
·          Rejea haraka iwezekanavyo.
·         Mchukulie zawadi
·         Jiepushe na kurejea nyakati zisizotarajiwa au nyakati za usiku.
·         Mchukue (safarini) ikiwezekana.


9.                  Msaada wa kifedha


·         Unatakiwa kuwa mtumizi kwa mujibu wa uwezo wake wa kifedha. Usiwe 
·         bahili na pesa zake (wala  usiwe mfujaji).
·         Unapata malipo kwa matumizi yote unayotumia kwa ajili ya kumkirimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha mkate ambacho unamlisha kwa  mkono wako  (hadiyth).
·         Unahimizwa  sana kumpa kabla yeye hajakuomba.


10.    Kunukia vizuri na kujipamba mwili

·         Kufuata Sunnah ya kunyoa nywele za  utupuni na   kwapani.
·         Daima uwe msafi na nadhifu.
·         Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)


11.    Jimai (Tendo la ndoa)

·         Unawajibika kulifanya mara kwa mara iwapo huna dharura (ugonjwa,n.k)
·         Uanze kwa “BismiLlaah” na du'aa zilizo sahihi.
·         Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi tu (sio sehemu ya nyuma)
·         Uanze kwa vitangulizi (vya jimai) ikiwa ni pamoja na maneno ya mapenzi.
·         Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.
·         Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza
·         Epukana na jimai wakati wa damu ya mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni haraam
·         Fanya chochote unachoweza kuepuka kuharibu kiwango chake cha haya alicho nacho (haya na staha) mfano kuvua nguo pamoja badili ya kumtaka avue yeye mwanzo huku ukiwa unamuangalia.
·         Epuka wakati wa jimai mkao ambao unaweza kumuumiza mfano kumgandamiza katika kifua inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe  ni mzito.
·         Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.


12.                  Kudhibiti Siri

·         Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa siri za  chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine  ya kibinafsi.


13.                  Kumuongoza katika kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)   


·         Muamshe katika sehemu ya tatu ya mwisho ya usiku kusali “Qiyaam-ul-Layl” (Swalah za ziada za usiku zenye sujuud na ruku’u za muda mrefu).
·         Mfundishe kile unachokijua katika Qur-aan na tafsiri zake.
·         Mfundishe “Dhikr” (njia za kumtaja Allaah kama alivyofundisha Mtume) za asubuhi na jioni.
·         Muhimize kutumia pesa kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama vile kutoa sadaka.
·         Mchukue katika safari ya Hijja na 'Umrah wakati unapokuwa na uwezo.


14.    Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zake

·         Mchukue katika matembezi kwa familia na jamaa, hususan wazazi wake.
·         Waalike kumtembelea na wakaribishe.
·         Wapatie zawadi kunapokuwa na jambo maalum (kama sikukuu)
·         Wasaidie wanapokuwa na haja kwa msaada wa fedha, nguvu, n.k.
·         Endeleza uhusiano mzuri na familia yake baada ya kifo  chake iwapo atakufa mwanzo. Pia kwa hali kama hii mume anahimizwa kufuata Sunnah na kutoa kile ambacho yeye (mke) alizoea kutoa wakati wa uhai wake kuwapa rafiki ya jamaa zake.


14.                  Mafunzo ya Kiislam na kumshauri kwa kumrekebisha


            Hii ni pamoja na:
·         Misingi ya Uislam.
·         Haki na wajibu wake.
·         Kusoma na kuandika.
·         Kumhimiza kuhudhuria darsa na halaqah(darsa duara za Msikitini na majumbani).
·         Hukumu za Kiislam zinazowahusu wanawake.
·         Kumnunulia vitabu vya Kiislam na kaseti kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.



16.       Wivu unaokubalika
·         Hakikisha kuwa anavaa hijaab kamili anapotoka  nyumbani.
·         Usimruhusu kuchanganyika ovyo na wanaume  wasio- Mahram.
·         Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano wake ni kama:

1.      Kulichambua kila neno na sentensi asemayo  na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo hakuzikusudia.
2.      Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.
3.      Kumzuilia kujibu simu, n.k.


17.    Subira na Upole

·        Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.
·         Hasira lazima zionyeshwe pale anapochupa mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), kwa kuchelewesha Swalah, kusengenya, kuangalia yasiyofaa katika TV, n.k.
·         Kumsamehe makosa anayokukosea wewe  (Angalia sehemu ya 18).
·         Ni namna gani unaweza kumrekebisha makosa yake?


1-   Kwanza, mpe ushauri kwa njia ya mzunguko na ya moja kwa moja mara kwa mara
 2-   Kisha kwa kumpa mgongo katika kitanda kumuonyesha hisia zako). Tanabahi kuwa hii  haihusishi kuhamia chumba kingine, kuhamia  nyumba nyingine, au kutomsemesha


3-   Utatuzi  wa mwisho ni kumpiga kidogo (kwa namna ilivyoruhusiwa) Katika hali hii, mume ni lazima aangalie yafuatayo

·        Ni lazima ujue kuwa Sunnah ni kuepukakumpiga kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumpiga mwanamke wala mtumwa

·        Ni lazima ufanye hivyo katika hali ya juu kabisa ya kutotii, mfano mara kwa mara kukataa tendo la jimai bila ya sababu, mara kwa mara kutosali kwa wakati wake, kuondoka nyumbani kwa muda mrefu bila ya ruhusa na kukataa kusema pahala alipokuwepo, n.k

·        Usifanye hivyo mpaka awe umeshampa  mgomo na kulijadili hilo suala pamoja nae kama ilivyoelezwa katika Qur-aan

·        Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza  au  kumpiga usoni au katika sehemu zilizo   nyepesi kuathirika katika mwili wake.


      ·        Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa kiatu, n.k.


18.    Kusamehe na makaripio yanayofaa

 ·        Mhukumu kwa makosa makubwa tu
 ·        Msamehe makosa aliyokukosea wewe bali mhukumu kwa makosa ya haki za Allaah, mfano kuchelewesha Swalah,  n.k
 ·        Kumbuka mazuri yote anayomfanyia kila wakati  anapofanya makosa
 ·        Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na umuwazie dharura mfano huenda amechoka, ana huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake katika Uislam bado yamo katika kukua   

 ·        Jiepushe na kumgombeza  kwa mapishi mabaya kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumlaumu yeyote katika wake zake kwa jambo hili. Iwapo amekipenda chakula, hula na iwapo hakukupenda hukiwacha na  hatoi maoni yoyote.
 ·        Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu wazi wazi
 ·        Epukana na kutumia jeuri au maneno yanayoumiza hisia zake
 ·        Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo subiri mpaka mnapokuwa faragha
 ·        Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii inasaidia kuweza kudhibiti maneno yako

0 comments:

Post a Comment